Kulingana na shirika la habari la Abna ukimnukuu Al-Quds, shirika la habari la Associated Press limearipoti kutoka kwa maafisa wa usalama kuwa roketi imegonga uwanja wa kuweka helikopta ndani ya Ubalozi wa Marekani.
Katika muktadha huo, chanzo cha usalama cha Iraki kwenye mazungumzo na Al Jazeera kimeasisitiza kuwa mfumo wa ulinzi wa anga wa ubalozi huo umelengwa.
Pia imeripotiwa kuwa radar iliyopo katika ubalozi huo imeharibika.
Baada ya Ubalozi wa Marekani huko Baghdad kulengwa, vyanzo vya habari vimeripoti kuhusu uharibifu wa mfumo wa ulinzi wa anga wa ubalozi huo.
Your Comment